Hello mulembe nation. I have a question. There’s a bachelor whose love interest’s grandmother is of the same clan as his own. Can they get married?
Hello mulembe nation.
Niko na swali.
Kuna kijana ako kwa uhusiano na msichana ambaye nyanya ya msichana (nyanya anayezaa mama ya msichana) ni ukoo mmoja na kijana.
Je, wanaweza wakaoana?
Hujambo Kaka?
Asante kwa swali lako. Pokoea salamu tele za pasaka kutoka kwetu sisi wote hapa mulembe nation.
Kulingana na mila za Kiluhya wapenzi hao wawili wako na ukoo wa karibu.
Hii ni kumaanisha kwamba hawawezi kuoana.
Nyakati za mababu zetu, iliamikia kwamba watoto watakao zaliwa kutokana na ndoa kama hiyo wata taabika kiafya haswa: kufura mwili, kupooza, ngozi kubadilika ikafanana na ya mfu, kudhoofika na hatimaye kufa.
Isitoshe, iliaminika kwamba kifo cha mapema kilikuwa tunda la kawaida kwa penzi kama hili la sumu.
Maafa haya yalichukuliwa kuwa adhabu kutoka mababu kwa kukiuka desturi na mila za Kiluhya kuhusu ndoa na mapenzi.
Kwa hivyo, ilikuwa kawaida kwa wapenzi kama hao kuwa na maisha mafupi duniani. Yani, kifo cha mapema kiliwa andama.
Lakini, ikiwa kuwa kwa njia moja ama ingine ingepatikana kuwa ndoa kati ya wawili walio na ukoo imeshafanyika kimakosa, basi mila za Kiluhya zilifanywa ili kupunguza mkali au kuwakinga wanaohusika kutokana na maafa.
Baadhi ya mila, desturi na itikadi za mapenzi na ndoa katika jamii ya Waluhya
Kwa mfano, kaitika jamii ya Maragoli, wazee wangechukua nyungu na kuivunja kwa ustadi fulani; lengo ikiwa ‘kinywa’ cha nyungu kibakie kikiwa umbo la mvirongo kama vile chanda (yaani ring shape kwa lugha ya kimombo).
Kisha, kipande hiki cha nyungu kingevikwa kwa paa la nyumba ya hao wapenzi haram. Kikamilifu, hapo juu ya kesegese.
Iliaminika kwamba kipitia tendo hili la kimila, kinga fulani ingewajia wapenzi hao amabao walikuwa wamekiuka itikadi za jamii za ndoa.
Kumbuka ya kwamba kwa Mluhya halisi, nyungu inachukuliwa kama ishara ya nyumba ya mtoto, yani uterus kwa kimombo. Hivyo hivyo kinywa chake ni cervix na ‘tumbo’ ikiwa sehemu ya nyumba ya mtoto ambayo kibiolojia inaitwa fundus.
Maana hii fiche ya nyungu kaitika jamii ya Waluhya ina umuhimu kadha wa kadha. Kwa mfano, kwa Wamaragoli ipo sherehe ya kurugiza; nao Wabukusu kipitia desturi zao kama vile umuhimu wa sikolonjo, wanashiria maana fiche na umuhimu wa nyungu kwa maisha ya Mluhya kamili.
Wasia wa Omwami Mwene
Ndugu, kulingana na swali lako, sidhani nitakosea sana nikisema kwamba kaka ambaye tunaongelea ni wewe mwenyewe.
Tukichukulia hivyo kwamba swali hili si la jumla, basi mawaidha yangu ni haya.
Inabidi kiasi cha haja na kikamilifu kutalakiana na mpenziwe. Ndoa au penzi lenyu ni haramu.
Kwanza, ndoa ni moja wapo njia amabzo Mluhya alidhibitisha ukoo.
Je, huyu mama ya mpenziwe utamuita senge au mama mkwe?
Pili, watoto wako wataitana aje na wa ukoo upande wa mama?
Kaka utakubaliana nami kwamba mambo haya si tu ya kukanganya bali na ya aibu pia.
Wako,
Omwami Mwene.
Subscribe to Mulembe Weekly
Get culture, language, stories and discussions in your inbox every Friday 5 PM East Africa Time